Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TUNDA LA UTU WEMA.

Wema wa Mungu kwa wanadamu.
1.Hili ni tunda ambalo linaonyesha wema wa Mungu kwa waovu na wenye haki, kwa sababu huwatendea  mema. Wakristo ambao wameokoka yawapasa kufanana na yeye kwa kuwatendea watu wote mema. “Ili mpate kuwa kama wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.”  Mt 5:45.
2.Vile vile ameonyesha wema wake kwa kutuokoa. “Lakini wema wake Mwokozi wetu  Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa.” Tit 3:4.

3.Anawavuta kwa wema wake ili wenye dhambi watubu. “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?” Rum 2:4.

Yatupasayo kuwatendea adui zetu.
1.Kuwasamehe na kuwaombea Baraka. “Wabarikini wanaowaudi; barikini, wala msilaani.” Rum 12:14. “Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.” Mt 5:44. “Watu wasiolipa  baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi Baraka.” 1Pet 3:9.

2.Kuwatendea mema. “Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Lakini, adui yako akiwa na njaa , mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.” Rum 12:17,20-21.

Kwa kufanya hivyo Bwana anakuwa upande wetu akitusaidia na kuwalipa kisasi adui zetu. “Usiseme, Mimi nitalipa mabaya; Mgojee Bwana, naye atakuokoa.”  Mit 20:22. “ Wapenzi,  msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.” Rum 12: 19.  Bwana hatakawia kulipa kisasi kwa sababu amesema, “Kisasi ni change mimi, na kulipa; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.” Kum 32:35.
                                                                                             
Sharti linalohusu kutenda wema
Mtu anapotenda wema si vema kujionyesha au kutangaza ili watu wafahamu. “Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye wa mbinguni.” Mt 6:1. Kutokana na andiko hili tunajifunza ya kwamba mema tuyatendayo ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Yeye pekee ndiye anayestahi kutukuzwa kwa yale mema tuyatendayo. Ndio maana Mungu ameonya akisema, “Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine....” Isa 42:8.

Malipo kwa watu watendao wema.        
Wataurithi ufalme wa Mungu. “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, njooni, mliobarikiwa na Bwana, urithini ufalme uliowekwa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chukula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni mkanijia.
  
Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, nilini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu, tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulikuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme akajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, mlivyowatendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio  wadogo, mlinitendea mimi.” Mt 25:31-40.

Malipo kwa watu wasiotenda wema.
Watahukumiwa na kuadhibiwa katika mateso ya moto wa milele. “ Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayaria Ibilisi na malaka zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama;

Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au kiu, au u mgeni, au u uchi  au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadri msivyowatendea mmojawapo wa hao walio wadogo hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”  Mt 25:41-46.

Maoni

Chapisha Maoni