Kuishi kwa amani ni jambo la muhimu sana katika maisha yako, ikiwa umekwisha kumpokea Yesu Kristo na Roho mtakatifu . Utaweza kuamua mambo mbalimbali kwa kumwomba Mungu akupe ufumbuzi. Neno la Mungu linasema; “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu...” Kol 3:15. Hapa ninatoa ushuhuda wangu, katika maisha yangu nimekutana na mambo magumu yanayohitaji maamuzi. Lakini kwa kuwa nilimwomba Bwana hakukawia, alinijalia kuwa na wazo la uamuzi wa kutoa, na ndani ya moyo wangu nilikuwa na amani. Na yote niliyoyatolea maamuzi yalikuwa ni sahihi sawasawa na mwongozo wa Mungu. Kufanya kazi kwa haki. Kama wewe ni mwalimu, daktari, kiongozi, mfanyabiashara, askari au unafanya kazi yoyote inakupasa kuifanya kwa haki. Kwa kufanya hivyo ndipo utakuwa na amani na utulivu moyoni mwako; na pia utakuwa na haki ya kumtumaini Mungu kama ilivyoandikwa, “Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa utulivu ...
Blogu hii imekuwa msaada kwa watu wengi. Wamelifahamu neno la Mungu na kuimarika katika kumjua Mungu. Washirikishe na wengine.