Tutaangalia katika somo hili jinsi Mungu anavyosema na watumishi wake. Kuna njia ambayo Mungu alitumia kusema na wana wa Israel kupitia watumishi wake wakati wa Agano la Kale na Agano Jipya ilikuwa ni kwa njia ya manabii. Mungu alipotaka kusema na wana wa Israel alimtuma nabii na kumwaagiza maneno ambayo atawaambia watu wake. Ndio maana imeandikwa, "Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu". 2 Petro 1:21. Kutokana na andiko hili linaonyesha wazi nabii yampasayo kuzingatia. Jambo la kwanza kwa mkristo au mtumishi aliyeokoka ni lazima atoe unabii kwa mapenzi ya Mungu (yaani kwa matakwa Mungu). Jambo la pili ili mkristo au mtumishi aliyeokoka aweze kutoa unabii ni lazima awe ameongozwa na Roho mtakatifu. Njia hii ni mojawapo tu lakini zipo njia nyingine ambazo Mungu hutumia kusema na watu wake ambazo ni kama ifuatavyo; 1. Kwa njia ya...
Blogu hii imekuwa msaada kwa watu wengi. Wamelifahamu neno la Mungu na kuimarika katika kumjua Mungu. Washirikishe na wengine.