Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU

Ahadi ya Mungu.
Mungu aliahidi kwa kinywa cha nabii Yoeli wakati wa agano la kale akasema nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili. Alikuwa anausemea wakati wa sasa ambao ni wa angano jipya. “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono, tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile nitamimina roho yangu” Yoeli 2:28,29.

Ni nani atampokea Roho Mtakatifu?
1) Anayetubu na kusamehewa.
“Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu” Matendo 2:38. 

2) Anayemtii Mungu. 
Anayemtii Mungu ni mtu yule aliyemwamini Yesu na kuokoka na kuweka nia ya kuishi sawa sawa na neno la Mungu, huyo hakika atampokea Roho Mtakatifu. “Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio” Matendo 5:32.

3) Aliye na kiu na kumwamini Yesu. “…Yesu akasimama; akapaza sauti yake akasema, mtu akiona kiu (kutamani), na aje anywe. Aniaminiye, kama vile maandiko yanavyonena, mito ya maji yalio hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminiye watampokea badaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa” Yohana 7:37-39.

4.Yampasa kukubali ubatizo halisi ambao Mungu alimtuma Yohana abatize watu kwa kuwazamisha ndani ya maji mengi. Haiwezekani kwa mtu ambaye anampinga Mungu kuhusu ubatizo halisi wa kuzamishwa katika maji mengi, halafu akampokea Roho Mtakatifu. Ni jambo la muhimu kufahamu ya kwamba ubatizo sahihi ni ule ambao Mungu alimwagiza Yohana hata akambatiza Yesu ili kutimiza majawapo ya agizo la Mungu. Kwa kuwa Yesu alikuwa anayafahamu maagizo ya Mungu alifundisha na kuonyesha ya kwamba ni jambo la lazima mtu azaliwe kwa maji na roho na ndipo ataingia mbinguni. Ndio maana, “Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” Yohana 3:5-6.

Maana ya kuzaliwa kwa maji na roho.
Kuzaliwa kwa maji ni wakati mtu anapobatizwa kwa​ kuzamishwa ndani ya maji mengi. Pia mtu huzaliwa kwa roho wakati ameamua kuokoka na  kumwamini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake kwa kutubu na kuziacha dhambi.  

Mtu anaweza kumpokea Roho Mtakatifu akiwa na imani na utakatifu. Kama mtu hana imani na utakatifu haiwezekani akampokea Roho Mtakatifu.  Siyo sahihi mwamini yeyote kufikiria​ ya kwamba mtu anaweza kujazwa Roho Mtakatifu kwa imani bila kuwa na utakatifu. Ni lazima mwamini awe na utakatifu kwa kuwa Roho Mtakatifu yeye ni Mtakatifu, hukaa na wale walio watakatifu. 

Ni wakati gani mtu anajazwa Roho Mtakatifu?
1). Mtu anajazwa Roho Mtakatifu wakati anapofanya maombi.
“Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu …” Matendo 4:31. Pia mtu anaweza kujazwa Roho Mtakatifu akiwa ananwabudu na kumsifu Mungu. Au wakati anapobatizwa.

Kinachotokea mtu anapojazwa Roho Mtakatifu
 1). Anapokea nguvu ndani yake na ujasiri wa kuwa shahidi wa Yesu. 
Anakuwa na nguvu ya kushinda dhambi, na ujasiri wa kuhubiri habari njema za ufalme wa Mungu.“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.…wote wakajaa Roho mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri” Matendo 1:8, 4:31.

2). Roho Mtakatifu anakaa ndani yake. “Ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala kumtambua; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu” Yohana 14:17.

3). Anasema kwa lugha nyingine. Anajaliwa na Roho Mtakatifu kusema kwa lugha nyingine. “Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka” Matendo 2:4.

Ni kwa nini Roho Mtakatifu alikuja kwetu? Majibu ya swali hili ni kama ifuatavyo:
1). Alikuja ili awe msaidizi wetu na kukaa nasi. Yeye anatusaidia katika maisha yetu mambo mengi. “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele. Ndiye Roho wa kweli…”Yohana 14:16, 17.   

2). Kutusaidia kuomba.
“Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu” Warumi 8:26, 27.

3). Kutuongoza na kutuambia mambo yajayo. “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatoa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu, kwa hiyo nalisema ya kwamba atatoa yaliyo yangu na kuwapashani habari” Yohana 16:13-15.

 “Kwa kuwa wote wanaongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” Warumi 8:14. Neno linaonyesha wazi wanaongozwa na Roho mtakatifu ni wana wa Mungu, ambao wamekwishafanyika watoto wa Mungu kwa kumpokea Yesu. “Bli wote waliompokea waliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” Yohana1:12.

4). Kutufundisha na kutukumbusha.
“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu,   atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” Yohana 14:26.

5). Kutumiminia pendo la Mungu katika mioyo yetu.
“…kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu aliyetupa sisi” Warumi 5:5.

6). Kuuhakikishia ulimwengu dhambi, haki na hukumu. 
“…huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu” Yohana 16:7,8.  Roho Mtakatifu anauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu wakati watumishi wa Mungu wanapohubiri na kufundisha neno la Mungu.     

7.Kutushuhudia kuwa watoto wa Mungu.
“Roho mwenyewe hutushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu.” Warumi 8:16. Ukiishi sawasawa na neno la Mungu Roho mtakatifu  anakushuhudia ndani yako ya kwamba wewe ni mtoto wa Mungu. Kama neno la Mungu linavyofundisha waliompokea Yesu walipewa haki ya kuwa watoto wa Mungu. Lakini haki hii hawakuipata bila kujitolea au kujikabidhi kwa Mungu. Walimgeukia Mungu na kuacha maovu yote kwa kutubu na kusamehewa, ndio maana walifanyika watoto wa Mungu.

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII.

Kutokana na kichwa cha somo hapa juu katika matukio wazi ili mtu amtumikie Mungu ni lazima awe na bidii. Kwa sababu hiyo kwa mtu yule ambaye ameweka nia moyoni mwake ya kwamba atatumikia Mungu kwa bidii. Tukiangalia kuhusu mwanadamu kuna mambo mengi katika maisha yake ameyafanya kutokana na bidii aliyo nayo. Lakini ikiwa mtu hana bidii kwa ajili ya mambo ya Mungu kamwe hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ndio maana imeandikwa;  "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatimkana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka,   Mathayo 11:12 ."    " Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu."   Luka 16:16. Hapa ninatoa ushuhuda wangu binafsi, kuhusu kumtumikia Mungu kwa bidii. Wakati nilipookoka nilikuwa na kiu au shauku kwa ajili ya kutaka kujazwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu nilikuwa ninamhitaji sana nilimwomba mtumishi mmoja wa Mungu aniombee ili niweze kujazwa...

KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU.

Utakatifu  - Ni maisha ya Mkristo anayoyaishi kwa kuzingatia kanuni ya neno la Mungu baada ya kumkiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kuishi maisha ya utakatifu ni jambo linalowezekana, kwa sababu Mungu alipomuumba mwanadamu alimwekea hiari ndani yake kwa kutokea kwa tukio. Ndio maana Yesu alipokuwa akifundisha alitumia mfano wa mti kuonyesha mtu anavyoweza kuishi maisha haya ya kumpendeza Mungu au ya maisha ya dhambi. "   "Ufanye mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana" Mathayo 12:33. Kuishi maisha ya utakatifu ni agizo la Mungu kwa wale wote aliowachagua. Ndio maana Mungu alimwambia Musa,   "Nena na makutano wote na wana wa Israel, uwaambie, mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu"  Walawi    19:2. Kuwa mtakatifu ni kumpendeza Mungu, kwa sababu amesema;  “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora...

TUNDA LA UAMINIFU.

Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho katika maandiko matakatifu. Tutajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika neno lake. Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana wa Israel bali kwa watu    wote wanaoishi sawasawa na neno lake. Kwa hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na kulitenda neno la Mungu.   “Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu.   Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako.”   Kum 7:9, 12.   “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu    halitanirudia bure bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.   Isa 55:11" Tabia ya mtu mwaminifu. 1. Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawa...